MTAHINIWA MKOANI MBEYA ANG'ATWA NA MBWA, AKOSA MSAADA WA MATIBABU BAADA YA KUKOSA FEDHA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MTAHINIWA MKOANI MBEYA ANG'ATWA NA MBWA, AKOSA MSAADA WA MATIBABU BAADA YA KUKOSA FEDHA.

 Mtoto VANESA AMBA mwenye umri wa miaka 13, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Ivumbwe wilaya ya Mbeya vijijini ameng'atwa na Mbwa mkono wa kuume/kulia na hivyo kupelekea kukosa msaada wa kupewa matibabu kwa kile kilichodaiwa kuwa alitakiwa kulipa shilingi 10,000/= mara baada ya kufika  katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Leo hii  Septemba 7 mtoto huyo anatakiwa kuanza Mitihani ya kuhitimu elimu ya Shule ya msingi, Na mpaka habari hii inaingia mtandaoni alikuwa hajapatiwa msaada wowote. Mtoto huyu analelewa na Bibi yake Bi GRENDINA FUNGO mwenye umri wa miaka 65 ambaye hajiwezi na hivyo kuomba msaada kwa wasamalia wema kuweza kunusuru maisha yake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages