Rais
Jakaya Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu
unaojumuisha wahandisi, Wabunifu majengo,
Wakadiriaji na Makandarasi uliofanyika Mlimai City Jijini Dar es salaam
jana
Rais
Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango
mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Dr. Ramadhani Dau akiwa mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa cheti
na Rais Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika
sekta ya ujenzi nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Dr. Ramadhani Dau(Wa Pili Kushoto) akiwa wkenye mkutano huo jana jijini
Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akiwa
katika Picha ya pamoja Mara baada ya kufungua Mkutano wa wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makandarasi
uliofanyika Mlimai City Jijini Dar es salaam jana
Na Alfred Ngotezi
Rais Jakaya Kikwete leo
amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo
katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Rais Kikwete ambaye alikuwa
mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha wahandisi,
Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba
ya Bodi ya Wakondrasi.
Mkutano huo uliohudhuriwa na
maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha
tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini,
Zambia, Kenya na Malawi.
Akiongea kwenye hafla hiyo
fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam,
Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi
walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata
uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Katika siku za karibuni NSSF
imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa
Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es Salaam na Zanzibar na
nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni NSSF itaanza kujenga
Daraja la Kigamboni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)