Meneja Miradi
Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo akikabidhi kwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi hundi ya
Sh.milioni 10 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya kusaidia
waathirika wa ajali ya Mv.Spice Islander. Hafla hiyo ilifanyika
mwishoni mwa wiki mjini Unguja.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu baada ya
kupokea mchango wa TBL, wa sh. mil. 10 za kusaidia waathirika wa ajali
ya Mv.Spice Islander. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini
Unguja.Katikati ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Zanzibar, Mweidady Mbaga baada ya kupokea mchango wa TBL, wa sh. mil.
10 za kusaidia waathirika wa ajali ya Mv.Spice Islander. Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Unguja.Kulia ni Meneja Miradi
Maalum wa kampuni hiyo, Emma Oriyo na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo,
Dorris Malulu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)