Mdau je unakumbuka enzi zile wakati zinaingia Televisheni?
ambapo kila atakayenunu Tv uswahilini ama mtaani kwenu basi kila mtu
atajua na majirahi walikuwa hawaishi kubisha hodi kuomba kuangalia
mchezo ama taarifa ya habari na wengine walikuwa wakijazana madirishani
kama uonavyo watu hawa pichani.
mini usiamini mambo haya bado
yapo katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam hadi leo hii, kama
walivyokutwa na kamera ya Sufianimafoto madada hawa wakichabo katika
dirisha msela aliyekuwa akicheki muvi geto kwake huko mitaa ya Mtoni kwa
Aziz Ali ni hivi majuzi tu.
Enzi
hizo hata wenye nyumba walikuwa wakikorofishana na wapangaji wao mara
kwa mara eti wengine wakitoa visingizio vya kumaliza umeme na wengine
utawasikia "mnatupigia kelele" kumbe jana yake alizuiliwa mtoto wa
mwenye nyumba kuingia kudeku Muvi katika chumba hicho cha mpangaji
mwenye Tv tene labla alizuia kutokana na kuwa na wageni kwa wakati huo
hivyo hakuhitaji usumbufu kwa wakati huo, lakini Mwenye nyumba tayari
sababu kibao na ugomvi na visa visivyoisha kwa mpangaji wako. Lakini kwa
sasa watu kidogo wameelimika na siku hizi kila mtu anajitahidi kuwa na
Tv ndani kwake ila katika baadhi ya kitaa bado mambo ni yale yaleeeeee!
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)