Mkurugenzi
wa Kampuni ya Shear Illusions na Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi Shear
Charity Ball,Shekha Nasser akiongea na waandishi (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam wakati akitanga kundi Kundi la wacheza Dansi wa
muziki wa Salsa la ‘Mutati Dancers’ toka nchini Kenya litakalo tumbuiza
siku ya tafrija ya hisani ya kila mwaka ya Shear (Shear Charity Ball
2011) yenye lengo ya kutunisha mfuko na kusaidia akina mama wenye
matatizo ya fistula katika hospitali ya CCBRT na pia kuwezesha ukarabati
wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka katika hospitali ya
Amana.Tafrija hii ya hisani itafanyika tarehe 01 Oktoba kuanzia saa moja
kamili jioni katika ukumbi wa Kivukoni, uliopo katika hoteli ya
Movenpick,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Bilicanas Group,Dk. Lilian Mbowe akionyesha moja ya
kipeperushi kinachoonyesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na kampuni
hiyo ambao ni moja ya wadhamini wa tafrija ya hisani ya kila mwaka ya
Shear (Shear Charity Ball 2011) yenye lengo ya kutunisha mfuko na
kusaidia akina mama wenye matatizo ya fistula katika hospitali ya CCBRT
na pia kuwezesha ukarabati wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka
katika hospitali ya Amana.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Precision
Air,Annette Nkini.
Mkurugeni
wa Kampuni ya Ulinzi ya G4s,Jacqui Bothma (kushoto) akizungumza katika
mkutano huo wa maandalizi ya tafrija ya hisani ya kila mwaka ya Shear
(Shear Charity Ball 2011) yenye lengo ya kutunisha mfuko na kusaidia
akina mama wenye matatizo ya fistula katika hospitali ya CCBRT na pia
kuwezesha ukarabati wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka katika
hospitali ya Amana.Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Huduma
kwa Wateja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Theopista Muheta na
kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Shear Illusions na Mwenyekiti Kamati
ya Maandalizi Shear Charity Ball,Shekha Nasser
Meneja
Uhusiano wa Precision Air,Annette Nkini akizungumza na waandishi wa
habari wakati katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Peacock
iliyopo katikati ya jiji la Dar.Precision Air ni mmoja ya wadhamini
wa tafrija ya hisani ya kila mwaka ya Shear (Shear Charity Ball 2011)
yenye lengo ya kutunisha mfuko na kusaidia akina mama wenye matatizo ya
fistula katika hospitali ya CCBRT na pia kuwezesha ukarabati wa mfumo
mzima wa maji safi na maji taka katika hospitali ya Amana.
Baadhi ya waanahabari ambao
ni wadau wa Shear Charity Ball wakifuatilia kwa makini mkutano.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)