![]() | |||
| Mwimbaji wa kundi hilo, Jokha Kassim, akiwa Studio kumalizia kurekodi wimbo wake wa Unavyojidhani Hufanani. |
Mpiga
Gitaa la Solo wa kundi hilo, Jumanne Ulaya, akicharaza gitaa wakati
wakimalizia kurekodi katika Studio za Bakunde Production.
**************************************
KUNDI
jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’
limekamilisha albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jila la Aliyeniumba
Hajanikosea, iliyoimbwa na Bi Mwana Hawa Ally, yenye jumla ya nyimbo
nne zilizorekodiwa katika Studio za Bakunde Production zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Mtandao wa Sufianimafoto, Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini,
alisema kuwa tayari wamekwishakamilisha jumla ya nyimbo nane ikiwa ni
sawa na albam mbili kwa mpigo.
Aidha
alisema pamoja na kukamilika kwa nyimbo za albam ya pili lakini bado
haijapewa jina kutokana na ukali wa kila wimbo uliomo katika albam hiyo
na kuwafanya kuwa na kigugumizi kuchagua jila albam hiyo ya pili.
Albam
hiyo inatarajia kuanza kuuzwa siku ya uzinduzi wa kundi hilo ambao
unatarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambapo
kwa sasa tayari nyimbo mbili zimekwisha sambazwa katika Vituo
mbalimbali vya Redio ili kuwasikilizisha mashabiki wa miondoko hiyo.
Kundi hilo linatarajia kurudi mjini Zanzibar kuweka Kambi na kuendelea na mazoezi yamaandalizi ya uzinduzi wao ambapo wanatarajia kuvunja Kambi rasmi siku mbili kabla ya uzinduzi.
“Tumeamua
kurekodi albam mbili kwa mpigo ili tuweze Kuwapa raha mashabiki wetu
pindi tutakapoanza kufanya maonyesho yetu ya majukwaani,
Na
pia baada ya tu ya kukamilisha zoezi hili la kurekodi sasa wasanii wote
watarejea mjini Zanzibar kuweka kambi na kuendelea na mazoezi hadi siku mbili kabla ya uzinduzi, tumeamua kufanya hivyo ili kuwafanya wasanii wetu waweze kufanya vitu kwa uhakika na kujiamini zaidi.” Alisema Amini
Alizitaja
nyimbo hizo zilizokwisharekodiwa kuwa ni pamoja na, Aliyeniumba
Hajanikosea, itakayobeba albam hiyo iliyoimbwa na Bi Mwanahawa Ally,
Unavyojidhani Hufanani, iliyoimbwa na Jokha Kassim, Mchimba Kaburi Sasa
zamu yake Imefika, iliyoimbwa na mkali wa BSS, Mrisho Rajab na Top
Bongo, iliyoimbwa Hassan Ally.
Nyimbo
nyingine ni, Riziki Shoti Kati, iliyoimbwa na Aisha Masanja, Umelisusa
Tembele Hela ya Nyama unayo, iliyoimbwa na Hasina Kassim, Majungu yenu
Kwetu ni Riziki, iliyoimbwa na Shinuna Kassim na Nipo Simpo, iliyoimbwa
na Mosi Suleiman.



Baadhi ya wasanii wa kundi hilo wakiwa katika Studio hizo wakimalizia kurekodi nyimbo za albam zao mbili.



No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)