Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) na Kamanda wa Kikosi cha
Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika
hizo kwa waandishi wa habari
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya
Mafuta ya Engen, Shaban Kayungilo na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha
Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika
hizo kwa waandishi wa habari
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ENGEN
kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia
baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha
usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani
inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.
Leo
tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu
itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Bukoba. ENGEN
Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni
ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la
Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama
barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza
kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka
Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji
uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya
jitihada za kuokoa maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa
kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake
katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia
barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya ENGEN
kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema
“kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama
Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa.
Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali
ikiwemo T shirt 2,200 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .
Matokeo
ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila
mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa
miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki
kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi
katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel
imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha
jitihada hizi”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza
Note:
Umuhimu
wa usalama barabarani hauwezwi kupuuzwa, kila siku tunashuhudia ajali
nyingi zikisababisha kupoteza maisha, wa Tanzania wengi, uharibifu wa
mali nyingi zenye thamani ya mamilioni. Zaidi ya mguso wa kibinadamu
utokanao na ajali za barabarani lakini pia maafa na majeraraha
yatokanayo na ajali za barabarani zinaleta athari za kijamii na
kiuchumi. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu 2,850
wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani. Takwimu za
mwaka 2010 zinaonyesha kwamba watu 3,582 walipoteza maisha huku majeruhi
wakiwa zaidi ya 20,000 wakati watembea kwa miguu na wapanda baiskeli
wakiwa hatarini zaidi.
Mwaka
2010 katika jumla ya ajali 22,750 gharama au hasara iliyotokana na
ajali za barabarani zinakadiriwa kufika bil 363. Hii ni athari kubwa
kiuchumi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)