STARTIME MEDIA NA PROMOSHENI YA KULA TANO LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

STARTIME MEDIA NA PROMOSHENI YA KULA TANO LEO

Meneja Masoko msaidizi wa kampuni ya ving'amuzi ya Startime Media Tanzania Ltd Bw. Davis Mwijage akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya kuwapata washindi wa zawadi mbalimbali wa Promosheni ya "Kula Tano" iliyochezeshwa leo na mwigizaji nguli wa filamu nchini Steven Kanumba ambapo washindi mbalimbali wamepatikana, hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya kampuni hio yaliyoko Mikocheni jijini Dar es salaam, kulia katika picha ni Mwigizaji Steven Kanumba.
Mkurugenzi wa bidhaa na Masoko Startime Media Tanzania Ltd Ashley Zhao katikati akiwa katika picha ya pamoja na Zuhura Meneja Masoko wa Kampuni hiyo na mwigizaji Steven Kanumba wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi wa zawadi za promosheni ya "Kula Tano" iliyofanyika leo.
Zuhura Meneja Masoko wa kampuni ya Ving'amuzi ya Startime Tanzania Ltd akiwa katika picha ya pamoja na Mwigizaji Steven Kanumba katikati pamoja na Ofisa wa Masoko wa kampuni hiyoEric Cprian.
Hawa ni vimwana wa huduma kwa wateja wa kampuni ya Startime Media Tanzania Ltd kutoka kulia ni Veronica Msaga, Aisha Sawa, Jaquline Muro .a Dorothea Mathew wakipozi kwa picha mara baada ya hafla hiyo kumalizika..Picha Na Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages