Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and
Barbuda Mh. Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika
sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha
usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf
Astoria jijini New York Jumatatu usiku.
(Picha kwa hisani ya Ikulu)
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais
Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa
Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Dkt Marion Bergam, Mkurugenzi
wa miradi ya Health Care Projects ya Miracle Corners of the World
katika mkutano wa kwanza wa kuhimiza hatua zichukukuliwe dhidi ya
magonjwa yasiyoambukiza, hususan ya kinywa. Serikali ya Tanzania ndiyo
iliyodhamini mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha New York kitivo cha
meno
Mwanamuziki
maarufu wa Afrika Kusini ambaye ni Balozi wa heshima wa Roll Back
Malaria Yvonne Chakachaka akiendesha shughuli hiyo kama MC
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)