Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwenyeji wakeRais Mwai
Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku moja
uliojadili tatizo la njaa na ukame linazozikabili nchi za pembe ya
Afrika uliofanyika katika kituo cha Umoja wa mataifa uliopo Gigiri, nje
kidogo ya jiji la Nairobi,Kenya jana asubuhi.
Wakuu
wa nchi walihudhuria mkutano wa ulijadili jinsi ya kukabiliana na
tatizo la njaa na ukame katika nchi za pembe ya Afrika.kutoka kushoto
ni Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini,Waziri mkuu wa Ethiopia Meles
Zenawi,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyopo Nairobi
Bi.Sahle Work Zewle, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia na Makmu wa Rais
wa Kenya Steven Kalonzo Musyoka.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Somalia Sheikh
Sharif Sheikh Ahmed jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa mkutano
uliojadili jinsi ya kukabiliana tatizo la njaa na ukame katika nchi za
pembe ya Afrika.Katikati ni mwenyeji wa mkutano huo Rais Mwai Kibaki
wa Kenya.
(Picha na Freddy Maro)
(Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)