Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein
(katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif
Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio
la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi
mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi
ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi
walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice
Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja
usiku wa kuamkia leo.
Baadhi
ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wnaharakati
wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali
ya kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya
Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Baadhi
ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium
Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo katika ajali ya
kuzama kwa Meli ya Mv SpiceIslander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi
Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
MAKAMU
WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AKIONGOZWA NA
NAIBU KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEKHE KHAMIS HAJI KHAMIS WAKITOKA NDANI YA
HEMA MAALUM LILILOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA KWA AJILI YA
KUPOKELEA MAITI ZA AJARI YA MV.SPICE ISLANDERS ILIYOKUWA IKITOKEA UNGUJA
KWENDA PEMBA USIKU WA KUAMKIA LEO.
BALOZI
SEIF ALI IDDI AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIWA WA KUFUATWA KWA WATU
WATAKAOKUJA KUANGALIA MAITI ZAO NDANI YA HEMA, HADI MUDA HUU TAYARI
MAITI MBILI ZIMESHA HIFADHIWA NDANI YA HEMA ILO TAYARI KWA KUTAMBULIWA
KATIKA MAANDALIZI HAYO IDARA YA MAAFA WAKISHIRIKIANA NA OFISI YA MUFTI
WA ZANZIBAR WATAZIHUDUMIA MAITI ZOTE KWA KUZIKOSHA,KUZIVIKA SANDA NA
KUZIKA
WATU
WALIOJAZANA KUANZIA UWANJA WA MAISARA HADI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA
WAKISUBIRI KUWATAMBUA MAITI ZAO,KARIBU MATAYARISHO YOTE YANAYO STAIKI
KUFANYIWA MAITI YAMEKAMILIKA KINACHOSUBILIWA NI UPOKEAJI WA MAITI,
TAYARI WATU WASIOPUNGUA 300 WAMEOKOLEWA WAKIWA WAZIMA WENGI WAO NI
WATOTO NA KINAMAMA.
Picha Na Habari Kwa Hisani Ya Latest News
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)