NIT WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA MAANDIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU KISEKTA YA UCHUKUZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NIT WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA MAANDIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU KISEKTA YA UCHUKUZI

Kapteni Mstaafu katika fani ya usafirishaji wa meli Thomas Mayagilo (kushoto) akiwafafanulia waandishi wa habari mambo mbalimbali baada ya kutoa mada yake katika mkutano wa sekta ya Wasafirishaji jijini Dar es Salaam Sept,16,2011 ikiwa ni katika maadhimisho ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru Tanzania Bara katika sekta ya Uchukuzi
Naibu Waziri wa uchukuzi Othman Mfutakamba akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athmani Mfutakamba (kushoto) pamoja na Mdau wa sekta ya Uchukuzi Mr, Awadh wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Wasafirishaji (NATIONAL LOGISTICS CONFERENCE) ( jijini dar es Salaam Sept,16,2011) ikiwa ni moja ya ratiba ya shughuli za maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya UHURU kwa Wizara ya Uchukuzi ,
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa National Logistics Conference Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athman Mfutakamba (katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya( NIT )Mhandisi Priscilla Chilipwali(Mwanamke) pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji ((NIT) Elifadhili Mgonja wakielekea kwenye chumba cha mkutano wa wadau wa Usafirishaji jijini Dar es Salaam (Sept 16,2011) ikiwa ni shughuli za maadhimisho ya miaka 50 ya UHURU kwa Wizara ya Uchukuzi ambazo zimeanza tarehe 14 Sept hadi 17 Sept.2011,
Wadau wa NIT wakipiga makofi baada ya Naibu waziri wa Uchukuzi Athman mfutakamba kuwafungulia mkutano.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usafirishaji (NIT) Florian Ifunya (kulia) akitoa maelezo kwa wadau wa sekta ya Usafirishaji waliohudhuria kwenye mkutanowa wadau wa Wasafirishaji jijini Dar es Salaam Sept,16,2011 lililofunguliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athumani Mfutakamba (hayupo pichani) ikiwa ni baadhi ya shughuli za maadhimisho ya miaka 50 ya UHURU kwa Wizara ya Uchukuzi kisekta, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages