Zaidi
ya wakazi 100 wa MTAA WA MIEMBE GIZA – KATIKA MLIMA WA KISEKE WILAYANI
ILEMELA JIJINI MWANZA WAMEAPA KUTOHAMA KATIKA ENEO HILO KUTOKANA NA
MWENYEKITI WA MTAA WA MIEMBE GIZA BWANA KAMANI KUVUNJA MISINGI YA NYUMBA
35 NA NYUMBA ZAIDI YA 100 WALIZOKUWA WAMEJENGA HIVYO KUWASABABISHIA
HASARA NA UPOTEVU WA MALI ILE HALI BAADHI YA NYUMBA WANAZODAI KUWA NI ZA
MATAJIRI ZIKIBAKIA KATIKA ENEO HILO BILA KUVUNJWA.Wakizungumza
na blogu hii katika eneo la tukio wananchi hao wamesema kuwa mnamo
mwezi September 3 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni Mwenyekiti wa mtaa
huo bwana Kamani akiongozana na watu wake kwa kutumia nguvu alibomoa
nyumba na misingi ya nyumba za wakazi hao hali ambayo wanadai ni makosa
na haikuwa sahihi.
Kupitia amri ya mwenyekiti wa kitongoji hicho nyumba nyingi
zimebomolewa, mali kuharibiwa na nyingine kupora huku baadhi ya wakazi
wa eneo hilo wakiachwa hawana mahala pa kujisitiri.Picha Na Unique Entertainment
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)