MAKAMU
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK, BILAL AKIWA NA MAKAMU WA
PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF WAKIMFARIJI MMOJA KATI WA WAHANGA
WA MV.SPICE ND MUSSA HEMED ANAETOKEA MJI WA WETE ALIYELAZWA KATIKA
HOSPITALI KUU YA MMNAZI MMOJA,
MAKAMU
WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI ALIPOMTEMBELEA MTOTO
SAID JERAD MMOJA WA MAJERUHI WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI
MMOJA, ZAIDI YA 600 WALIOKOLEWA WAKIWA HAI KUFUATIA KUZAMA KWA MELI YA
MV. SPICE
Baadhi ya abiria 525 waliookolewa
kutoka katika Meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi Zanzibar
wakiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar
Watoto
waliookolewa kutoka ktika Meli iliozama ya Spici huko katika mkondo wa
Nungwi zanzibar wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kabla ya
kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Umati wa watu wakiwa katika
Hospitali ya mnazi mmoja kupata taarifa za watu wao kuhusiana na kuzama
kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa Taasisi zilizokuwa mstari wa mbele
katika harakati za uokoaji na usafirishaji wa maiti zilizopatikana
kutoka katika meli iliozama ya spici iliokuwa ikielekea Pemba, kama
wanavyoonekana katika picha.
Mmoja
kati ya waokozi akiwa katika hali ya majonzi baada ya kuchukuwammoja
kati ya maiti zilizoletwa bandarini zanzibar na chombo cha bawe kutoka
katika meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi.
Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na
Naibu kadhi wa Zanzibar kutokana na msiba mkubwa uliotokea zanzibar
jana.
Makamo
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akizungumza na Madaktari
huko katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar kuhusiana na Msiba
mkubwa ulolikumba taifa letu la kuzama kwa meli ya Spici huko katika
mkondo wa Nungwi kaskazini unguja.
Madaktari,Wauguzi na watu mbalimbali
wakipokea maiti ya kwanza iliofikishwa huko katika viwanja vya Maisara
kutoka katika meli ya spici iliozama hapo jana huko katika mkondo wa
Nungwi. PICHA ZOTE NA
HAMAD HIJA-MAELEZO ZANZIBAR
Na
Hamad Hija Maelezo zanzibar
MAMIA
ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya
Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili
kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao ambao walikuwepo katika
meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana
Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali
za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo
mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba
kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba
Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya
wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia
kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema
kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo
zilichangia tukio hilo
Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa
kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa
umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua
vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu
Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika
bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa
wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo
Kufuatia ajali hii hiiitakuwa mara ya pili katika pindi cha
nyuma meli ya MV Fathi ilizama ambapo watu kadhaa wafariki dunia na
baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma
Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa
wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke
hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo
uliotokea hapa zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)