Mwendesha
mashua bora wa Afrika Mashariki Al Bush akipokea kikombe chake cha
ushindi kutoka kwa Benjamin Mariki Meneja wa vinywaji vikali kutoka
kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL), mara baada ya kuwashinda
waendesha mashua wenzake kutoka nchi 15 katika mashindano ya Johnnie Walker THE LASER OPEN COMPETITION yaliyoanza
juzi na kumalizika leo kwenye klabu ya Dar es salaam Yacht Club (DYC)
Masaki jijini Dar es salaam.
Mwendeshaji huyo wa mashua Bw. Al Bush amesema amekuwa akiendesha mashua
kwa muda wa miaka 25 sasa na amekuwa mshindi katika mashindano hayo kwa
miaka 9 katika mashindano yaliyofanyika nchi mbalimbali za Afrika
Mashariki.
Katika picha kulia ni anayeshuhudia ni Hellen Rattansi Meneja Mauzi na
Masoko.
Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers SBL ndiyo iliyodhamini mashindano
kupitia vinvywaji vyake vikali vya John Walker na yaliomalizika leo
jijini Dar es salaam
Bw
Richard Hamer akipozi kwa picha mara baada ya kupokea zawadi yake ya
chupa ya kinywaji (WINE) kutoka kwa Tom Vanneste katikati mratibu wa
mashindano hayo, kushoto ni Hellen Rattansi Meneja Mauzi na Masoko.
Hellen
Rattansi Meneja Mauzo na Masoko akimkabidhi Ype Smit zawadi yake ya
kinywaji cha Wine mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Johnnie Walker THE LASER OPEN COMPETITION yaliyomalizika leo jijini Dar es salaam
Meneja
Masoko wa Serengeti Breweriers Emilian Rwejuna kulia akikabidhi zawadi
Mwambao Jumbe Mmjoa wa washiriki wa mashindano ya kuendesha mashua Johnnie Walker THE LASER OPEN COMPETITION.
Kutoka
kulia ni Hellen Rattansi Meneja Masoko na Mauzo, Benjamini Mariki
Meneja wa Vinywaji vikali vya John Walker, Emilian Rwejuna Meneja Masoko
(SBL) na Mark Hart Real Comodole Sail (DYC).
Kutoka
kulia ni Meneja Masoko wa Serengeti Breweriers (SBL) Emilian Rwejuna ,
Benjamin Mariki Meneja wa Vinywaji vikali vya Johnnie Walker na Tom
Vanneste Mratibu wa Mashindano hayo wakijadiliana jambo wakati wa utoaji
zawadi kwa washindi wa shindano hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)