Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya
reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Uchukuzi miaka ya
nyuma, Job Lusimbe, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika
ujenzi na maendeleo ya Reli ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya
Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka
50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14
katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mzee John Nchimbi na mkewe, Sylviaa Nchimbi,
waliokuwa ni abiria wa kwanza kusafiri na Reli ya TAZARA mwaka 1976,
ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya
Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli
ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Mzee
Nchimbi na mkewe wamepewa zawadi ya kusafiri na treni ya TAZARA bure
katika kipindi chote cha maisha yao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah
Shekimweri, wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho
ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara na maadhimisho ya miaka 50
ya Uhuru wa Tanzania katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam leo
Septemba 14.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoka katika moja ya mfano wa Behewa la Daraja la kwanza la Treni ya
TAZARA, wakati alipokuwa katika maonyesho ya TAZARA, wakati wa
maadhimisho ya miaka 35 ya shirika hilo sambamba na maadhimisho ya
miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, iliyofanyika katika viwanja vya TAZARA
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah
Shekimweri, kuhusu matumizi ya Kibelenge wakati alipokuwa akitembelea
katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka
35 ya reli ya TAZARA kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa
Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya
Tazara jijini Dar es Salaam.
Makamuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu mataluma ya Reli na matumizi yake wakati
alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya
Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA, kuelekea maadhimisho ya miaka
50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14
katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)