NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Jumla
ya maiti 202 tayari zimepatikana katika ajali ya Meli ya Mv.Spice
Islander iliyotokea hivi karibuni huko Nungwi hadi hapo jana.
Maiti
tano zaidi zilipatikana hapo jana sehemu ya Shimoni Mombasa Kenya
ambapo maiti zote hizo zilizikwa huko huko Kenya kutokana na hali ya
maiti zilivyo ambapo kabla ya jana maiti 197 zilikuwa zimepatikana.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa
Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed zilieleza kuwa aliwasiliana na
Balozi mdogo wa Tanzania Nchini Kenya na kumthibitishia kwamba
isingewezekana kuwasafirisha maiti hao kuwaleta Zanzibar kwa ajili ya
kutambuliwa na jamaa zao kutokana na hali ilivyokuwa.
Amesema
maiti hao mmoja inakadiriwa ni miaka minane, mwengine miaka 20 hadi 25
na wengine miaka 40 wote ni wanaume na mtoto mchanga mwanamke
anakadiriwa na umri wa mwaka mmoja na nusu ambao wamepatikana katika
kijiji cha Diani.
Kazi
ya uokoaji bado inaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa vikosi vya ulinzi
na usalama, raia wa Tanzania pamoja na kikosi maalum cha Uokozi kutoka
Afrika ya Kusini.
Wakati
huo huo michango ya Rambi rambi inaendelea ambapo hapo jana Isnaashir
imetoa jumla ya Shl. Milion 30, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wametoa shl. Milion 15 Wabunge wa Afrika Mashariki wamechangia Milion 2
na Benki ya NMB imekabidhi hundi ya Milion 20.
Fedha
zote hizo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maafa ya kitaifa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar.
Shughuli
za uchangiaji bado zinaendelea na wananchi pamoja na Taasisi
mabalimbali za binafsi na Serikali zinaendelea kutoa michango yao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)