MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwasili katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages