MKAPA ALIPOZINDUA KAMPENI ZA CCM VIWANJA VYA SOKOINE IGUNGA JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKAPA ALIPOZINDUA KAMPENI ZA CCM VIWANJA VYA SOKOINE IGUNGA JANA

Mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga Bw. Kafumu Peter Dalali akiongea na wananchi wa jimbo la Igunga, katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho wakati wa kuomba kura kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sokoine mjini Igunga.
Rais Mstaafu na mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Wiliam Benjamin Mkapa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Igunga kupitia CCM Bw. Kafumu Peter Dalali, katika mkutano uliofanyika leo kwenye viwanja vya Sokoine.
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akiongea na wanaIgunga leo katika mkutano ho.
Kiongozi wa kundi la TOT na Mbunge wa jimbo Mbinga Magharini Kapten John Komba akiimba kwa pamoja na wanamuziki wenzake wanafuatia katika picha Dokii Wenslaus, Hafsa Kazinja na Mbunge wa viti maalum CCM Vick Kamata.
Kundi la Orijino Komedi likifanya vitu vyake katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoine mjini Igunga.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga Rostam Aziz akiongea na wana Igunga wakati alipokuwa akimuombea kura mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM Kafumu Peter Dalali.
Benjamin Mkapa Mzee wa Ukweli na Uwazi akiwamwagia sera wana CCM waliohudhuria katika mkutano huo.
Mbunge Kapten John Komba akiteta jambo na mbunge mwenzake Vick Kamata.
Vijana mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo kutoka matawi mbalimbali ya CCM wakiingia katika viwanja vya Sokoine mahali ambapo pamefanyika mkutano huo wa kampeni.
Wana Igunga wakinyanyua mikono yao juu juu wakati Mzee Benjamin Mkapa alipokuwa akihutubua mkutano huo.Picha Na John Bukuku

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages