Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh
Lazaro Nyalandu( Kulia),Mbunge wa Vunjo Mh Augustine Mrema ( Katikati)
na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mussa Samisi wakizungumza na vyombo vya
Habari mara baada ya kutazama sukari iliyokamatwa katika maeneo ya
mipakani Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya mifuko ya sukari iliyokamatwa
ikiwa imehifadhiwa katika ghala la Polisi kituo cha Polisi Himo Mkoani
Kilimanjaro.
Mkuu wa Kituo cha poliosi Himo Afande
Majura( Kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh
Lazaro Nyalanmdu na Mbunge wa Vunjo Mh Mrema baadhi ya magari
yaliyokamatwa yakiwa na bidhaa mbali mbali za magendo ikiwemo sukari.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh
Lazaro Nyalandu( Kushoto), akijibu hoja mbali mbali za Mbunge wa Vunjo
Mh Augustino Mrema (Kulia) alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea
Masoko na vituo vya biashara mipakani kastika Mkoa wa Kilimanjaro.
Wanaoshuhudia ni viongozi na watendaji wa Mamlaka mbali mbali katika Mji
Mdogo wa Himo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh
Lazaro Nyalandu akitoa maagizo kwa watendaji wa mamlaka mbali za
serikali katika Mji mdogo wa Himo mara baada ya kukamilisha ziara yake
ya kutembelea na kukagua masoko na vituo vya Biashara mipakani katika
Mkoa wa Kilimanjaro.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)