Mwimbaji wa kundi
hilo, Mrisho rajab, akiwa katika moja ya mazoezi ya kundi hilo hivi
karibuni.
mwimbaji wa kundi
hilo, Joha Kasim, akiwa katika moja ya mazoezi ya kundi hilo hivi
karibuni.
Baadhi ya wasanii wa
kundi hilo wakiwa katika Bandari ya Dar es Salaam wakati wakiondoka
jijini kuelekea Kambini Unguja, hivi karibuni.
Mwimbaji wa kundi
hilo, Hassan Ally, akiwa katika moja ya mazoezi ya kundi hilo, hivi
karibuni.
Na
Mwandishi
Wetu
KUNDI
jipya
la Taarab linalokwenda kwa jina la Tanzania Modern Taarab (T-Moto)
limesogeza
mbele uzinduzi wake uliokuwa ufanyike Septemba 30 mwaka huu hadi Oktoba
28.
Kundi
hilo
lililoondoka jijini na kuweka kambi ya maandalizi katika Visiwa vya
Zanzibar hivi
karibuni, limeamua kusimamisha mazoezi yake kwa muda wa wiki moja na
nusu
kufuatia msiba mkubwa ulioikumba nchi kutokana na ajali ya meli ya Spice
iliyozama eneo la Nungwi hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu
wengi na majeruhi ikiwa ni idadi ambayo haijawahi
kutokea katika Visiwa hivyo.
Akizungumza
na
mwadishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini,
ambaye ni
mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Salmini Amour ‘Komandoo’, alisema
kuwa
kutokana na kundi hilo kutambua ukubwa wa msiba huo ulio na idadi kubwa
ya vifo
vya watu kulinganisha na idadi ndogo ya watu waishio visiwani humo,
wameamua
kusitisha kambi ya mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya kundi hilo kuwa katika
maombolezo.
Aidha
amesema
kuwa wasanii wa kundi hilo wataendelea kubaki kambini bila kuendelea na
mazoezi hayo ya maandalizi ya uzinduzi wao, hadi baada ya wiki moja
na nusu kuanzia siku ya kwanza kati ya tatu za
maombolezo zilizotangazwa na Serikali ya Zanzibar.
Kundi
hilo
linatarajia kuwasili jijini wiki ijayo kwa ajili ya kuingia studio
kurekodi
nyimbo zake mbili zilizokwisha kamilika na kurejea tena Zanzibar
kuendelea na
kambi hiyo.
“Kwa
vile
tayari kundi langu lilikwishakamilisha baadhi ya nyimbo, litakuja jijini
wiki
ijayo kurekodi nyimbo mbili na baada ya kumalizo zoezi hilo watarejea
Unguja
kuendelea na kambi ili kukamilisha mengi kati ya mazuri
tuliyojipanganayo
kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa Taarab siku hiyo ya uzinduzi, Oktoba
28,
Na
pia
tumeamua kusogeza uzinduzi wetu tarehe ya mbali zaidi ili kuweza kufanya
maandalizi ya kutosha baada ya kusitisha mazoezi yetu kwa muda wa wiki
moja na
nusu kwani msiba huu ni wa kitaifa na ni mkubwa uliotugusa kila mmoja
wetu ili
kuepuka kuwakera watu kwa kufanya uzinduzi katika tarehe tuliyokuwa
tumeipanga
ambayo ilikuwa ni mwezi huu ambao bado tunamajonzi” alisema Amini
Baadhi
ya
wanamuziki wanaounda kundi hilo ni pamoja na , Mwahawa ally, Joha Kasim,
Mrisho
Rajab, Jumanne Ulaya, Hassan Ally, Mosi Suleiman, Rajab Kondo, Fadhili
Mnara,
Moshi Mtambo, Ally Kabura, Sabha, Rahma Asha Masanja na Hanifah Kasim.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)