Mshambuliaji wa Sunderland Asamoah Gyan aliifungia Ghana bao la kwanza kwa
kichwa katika dakika ya nane.
Emmanuel Agyemang-Badu akaongeza bao la pili katika dakika ya 78 baada ya
kuachia mkwaju wa umbali wa yadi 20. Hata hivyo ushindi huo wa Ghana uliingia dosari kutokana na kuumia kwa
mshambuliaji wao Gyan na alitolewa nje ya uwanja kabla ya mapumziko kutokana na
kile kilichoonekana maumivu ya msuli wa paja.
Sasa kuna wasiwasi kama ataweza kucheza mechi ya siku ya Jumanne dhidi ya
Brazil mjini London.
Black Stars ingeweza kushinda kwa mabao mengi lakini mkwaju wa nguvu wa
Kwadwo Asamoah alioufyatua kiasi cha yadi 30 katika dakika za nyongeza
ulipogonga mwamba na kutoka nje.
Matokeo hayo yana maana Black Stars inaongoza kungi lao kwa kukusanya pointi
13 huku wakibakiwa na mchezo mmoja tu.
Sudan wanaoshikilia nafasi ya pili, ambao wamezoa pointi 10, hawana budi
kuwalaza Congo mjini Brazzaville siku ya Jumapili ili waweze kuwa karibu kabisa
na Black Stars.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)