Wapenzi wa kinywaji mahiri
cha Guinness na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu nchini Tanzania, kwa mara ya
kwanza GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ itazinduliwa SEPTEMBA 4 katika viwanja vya Leaders Club. Usikose
kujionea maajabu ya mpira wa miguu katika kipindi hiki kabambe cha Televisheni
ambacho kinaangaliwa na kuwavutia watu wengi barani Afrika, ambapo kitawapatia
mashabiki nchini Tanzania nafasi ya kujitokeza na kuonyesha mapenzi yao ya dhati
katika mpira wa miguu na kushindana na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu
kutoka Kenya na Uganda na kujishindia mamilioni ya fedha.
Timu ya majaji itakuwepo
kwenye viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kufanya usaili kutafuta mashabiki
wenye mapenzi na vipaji kwa mpira wa miguu watakaoiwakilisha Tanzania katika
kipindi cha Televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
Kipindi cha Televisheni
cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ni cha kimataifa, Timu ya Majaji imeshafanya
usaili katika miji mikubwa ya Kampala, Nairobi na itakuwa Dar es Salaama tarehe
4 Septemba 2011 kwa ajili ya kutafuta mashabiki wenye mapenzi na vipaji kwa
mpira wa miguu kutoka nchi za Uganda, Kenya na Tanzania ambao watashindana ili
kupata nafasi ya kujishindia zawadi nono.
Mashabiki watakaotaka
kushiriki wanatakiwa waje na rafiki na wawe tayari kuonyesha uwezo wao.
Washiriki ni lazima wawe wawili wawili, mmoja kati yao inabidi awe tayari
kuonyesha kipaji na ujuzi wake wa mpira wa miguu na mwingine kuoyesha ufahamu
wake wa mpira wa miguu. Majaji wataangalia uwezo wako wa kuchezea mpira kupitia
mifumo ya mazoezi ya mpira wa miguu kuona ili kuona kama una uwezo na kipaji cha
kuingia katika kipindi cha televisheni cha Gunness Football Challenge.
Itakuwa ni siku nzuri kwa
kila mtu, kutakuwa na shughuli nyingi za mpira wa miguu, muziki na burudani,
Usikose nafasi hii ya kuwa mshiriki na kushuhudia maajabu ya mpira wa miguu
ambayo yatainyanyua nchi yetu. Njoo leaders tarehe nne mwezi wa tisa viwanja vya
Leaders Club kuanzia saa nne asubuhi. Watakaoruhusiwa kuingia ni wale wenye
miaka zaidi ya kumi na nane. Hakuna Kiingilio.
Kipindi cha GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™ kinakuja Tanzania, jitokeze na uonyeshe uwezo wako ili upate
nafasi ya kushinda hadi dola za kimarekani Elfu Hamsini kila wiki kwa wiki nane
kwenye kipindi cha television. Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha jirani zetu
Kenya na Uganda kuwa mashabiki wakubwa na mahiri wa mpira wa miguu wanatokea
Tanzania.
Tafadhali kumbuka, usinywe
pombe kupita kiasi. Guiness haiuzwi kwa
walio chini ya miaka 18
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)