DK SHEIN ZIARANI CHAKECHAKE NA ZIWANI PEMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DK SHEIN ZIARANI CHAKECHAKE NA ZIWANI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed shein,akizungumza na wananchi wa Ziwani Pemba, waliofili na jamaa zao katika ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja hivi karibuni,(kulia) ni Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya umoja wa Kitaifa waliofutana na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,katika ziara maalum ya kuwafariji wananchi walifiliwa na ndugu zao,katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed shein,na Mama Mwanamwema Shein,wakisalimiana na wananchi wa Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba wakati walipofika kuwafariji wananchi wa sehemu hiyo waliofiliwa na ndugu zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed shein,akiteta jambo na Waziri wa wizara Ardhi,Makaazi ,Maji na Nishati,mara baada ya kuwafariji wananchi wa Maziwani Pemba, waliofiliwa na ndugu zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi. Credits: Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages