VODACOM TANZANIA YAFIKISHA WATEJA MILIONI 10 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM TANZANIA YAFIKISHA WATEJA MILIONI 10

Vodacom Tanzania inapenda kuwashukuru sana watanzania wote na hasa wateja wetu kwa kuendelea kushirikiana nasi hadi hivi sasa tumefikisha wateja milioni 10.
Tuna kila sababu ya kuendelea kuwashukuru wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kwa uaminifu na mchango wao mkubwa wanaoendelea kuuonyesha kwetu kwa kipindi chote cha miaka 11 sasa.
Mafanikio mbalimbali tuliyoyapata hadi hivi sasa ni matokeo ya kuelewa mahitaji muhimu ya wateja wetu na kuhakikisha kuwa tunayatimiza na kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia huduma zetu.
Kama tulivyowaahidi wakati wa mabadiliko ya muonekano wetu, tunapenda kuwasisitizia kuwa tutaendelea kuyatimiza yale yote tuliyowaahidi na kuyaboresha zaidi.
Vilevile, tunawahakikishieni kuwa tutaendelea kuwa mtandao ulio bora na unaotoa huduma na bidhaa za bei nafuu zaidi hapa nchini.

Ripoti ya idadi ya wateja kama ilivyotolewa na TCRA

Mtandao Vodacom Airtel Tigo Zantel TTCL Sasatel Benson
Wateja 10,000,000 5,927,417 4,671,263 1,354,098 226,153 8,498 2,074

Ahsante Tanzania.
Vodacom, kazi ni kwako

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages