Mkazi wa Kinyenze katika Kijijin cha Kipera, Shabani Magua akizungumza katika mkutano wa Hadhara kijijini hapo.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara Kijijini hapo, hivi karibuni.
---
Na Mwandishi Maalum
WANANCHI
wa Kijiji cha Kipera Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero mkoani
Morogoro wamekilalamikia kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mvomero Bi. Euphrasia Buchuma kwa kushindwa kuwapa ufafanuzi
wa kina juu ya umiliki halali wa Mwekezaji aliyechukua mashamba yao na
kuziba njia kijijini hapo jambo ambalo limezi kuchochea mgogoro uliopo.
Wakizungumza
kijijini hapo muda mfupi baada ya kumlizika kwa kikao baina ya
Mkurugezni huyo, Mwekezaji Tanbreed Poultry Ltd, maofisa wa ardhi na
Wananchi wamesema alichofanya Mkurugenzi huyo ni kuja kuwalaghai tu na
si kuwapa ufumbuzi wa mgogoro huo.
“Huyu
Mkurugenzi inavyoonesha ni wazi yupo upande wa mzungu (mwekezaji) na
hata haiwezekani waje hapa badala ya kusikiliza pande zote mbili wao
wasome tu hati ya mwekezaji na kisha waseme ni halali,” alisema Mwajuma
Idd.
Aidha
inadaiwa kuwa licha ya Kijiji hicho kutakiwa kupeleka vielelezo vyote
vinavyoonesha kuwa Umiliki wa eneo hilo sio halali lakini Kiongozi huyo
na wote alioambatana nao walishindwa kusoma vielelezo vyao na hata
walipo hoji hawakupewa majibu ya uhakika jambo ambalo lilizidisha jazba
na kuchochea zaidi mgogoro huo badala ya kutatua.
Pia
wanamtuhumu Mkurugezni huyo kuwa anatumiwa na mzungu kuwanyanyasa
wananchi kwaa kitendo cha kushindwa kujadiliana naa mwekezaji huyo
katika kutano wa hadhara juu ya kufungua njia iliyofungwa kijijini hapo
hadi pale alipoenda nae ofisini kwake wakaenda kuzungumza.
“Hii
ni wazi kuwa kiongozi huyu anamanufaa yake hapa na ndio maana kashindwa
kuzungumza nae hapa hadharani na kuamua kwenda kuongea nae ofisini na
tutajuaje kama hakupewa hela kule?...sisi hatukubali na wala hatumtaki
mwekezaji huyu hapa kijijini, Joseph Sugu.
Nae
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kinyenze ambapo mgogoro huo wa ardhi upo,
Bwana Endeni Msangi amesema wao kama Kijiji hawajakubaliana na maekezo
ya Mkurugenzi huyo na wamepanga kuitisha mkutano wa Hadhara wa wananchi
wote kujadili hatua za kuchukua dhidi ya mwekezaji huyo.
“Viongozi
tumekubaliana kuitisha mkutano wa hadhara na kujadili na wananchi kuwa
nini kifanyike baada ya majibu ya kuzubaisha na kejeli ya mkurugenzi
ambayo kiukweli yamezidisha hasira ya wananchi dhidi ya mwekezaji
huyu,” alisema Msangi.
Miongoni
mwa hatua wanazopanga kuchukua ni pamoja naa kupinga kuwapo kwa
mwekezaji huyo kijijini hapo na wanadhamiria kwrnda mahakamani
kusitisha shughuli zote shambani humo hadi haki itakapo tendeka.
Wananchi
wa Kijiji cha Kipera Kitongiji cha Kinyenze wapo katika mgogoro wa
Ardhi na Mwekezaji wa kizungu aliyenunua ardhi kijijini hapo na kuvamia
mashamba ya wananchi, makazi na kufunga barabara inayounganisha
vitongoji.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)