Profesa Mbele
---
Profesa
Mbele akizungumzia kambi ya vijana 384 wa CCM waliopata mafunzo ya
kuwaongezea morali wa kukitetea chama Igunga. Profesa Mbele anasema;
"Hivi
ni vikundi vya fujo. CCM mna historia ndefu ya kusababisha fujo nchini,
kuanzia zile fujo za Visiwani, ambazo zilisababisha maafa na aibu kwa
Tanzania na pia wa-Tanzania kukimbilia Kenya na hadi Somalia. Bado
hamjakoma.
Kumbukeni kuwa idadi ya wa-Tanzania ambao ni wanachama wa vyama vya siasa ni ndogo ikilinganishwa na sisi tusio na vyama. Msidhani kuwa hii nchi ni yenu peke yenu, wala msidhani kuwa mna haki zaidi kuliko sisi ambao hatuna vyama.
Papo hapo, mngekuwa na busara, mngeiga mfano wetu sisi tusio na vyama,ambao tunalinda heshima ya nchi, wala hatuhujumu amani.
Nawashutumu vikali kwa sera zenu za kuwa na hivi vikundi vya fujo."

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)