MWAKILISHI
wa Viti maalum na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan
Juma, akimkabidhi shilingi milioni mbili, Makamu wa Pili wa Rais kwa
niaba ya Wabunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki kusaidia waathirika wa
ajali ya meli iliyotokea wiki iliyopita huko Nungwi.
RAIS
wa Shirikisho la Jumuia ya Waislamu wa Khoja Shia Ithna-Asher Afrika
Mashariki, Alhajj Anwarali Daramsi, akimkabidhi hundi ya shilingi
milioni thelathini, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Iddi kwa ajili ya kusaidia maafa ya kuzama kwa meli.
SPIKA
wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, akimkabidhi
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, msaada wa
shilingi milioni 15 kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo kusaidia wathirika wa ajali ya meli iliyotokea Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
AFISA wa
kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Shy-Rose Bhanji kulia, akimkabidhi
mfano wa hundi ya shilingi milioni 20, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia watu walioathirika
katika ajali ya meli iliyotokea wiki iliyopita katika mkondo wa Nungwi.
Kushoto Meneja wa NMB tawi la Zanzibar, Mluku Abdallah.
MKURUGENZI
wa Kampuni inayotoa huduma kiwanja cha Ndege cha Zanzibar (ZAT),Tobi
Marhun (kushoto), akimkabidhi shilingi milioni kumi Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Seif Iddi, kwa ajili ya waathirika
wa ajali ya meli ya MV. Spice Islanders wiki ilioyopita. Kulia
Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Mohammed Raza.Picha Zote na Othman
Mapara-Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)