Ajali hii
imetokea Majira ya Saa 2 na dakika 45 usiku, wakati dereva wa gari hilo
aina ya Lori kwa lugha nyingine Tipa au gari la kubebea Mchanga
akijaribu kumkwepa Mwendesha baiskeli na kulivaa gari kubwa la Mizigo
lilokuwa limepaki jirani na Kituo cha mafuta cha ORXY mtaa wa Mama John
Jijini Mbeya..
Jitihada ya
kuzipata namba za usajili wa ghari hilo ziligonga mwamba baada ya
kutolewa muda mfupi tuu toka kupata ajari.
Aliyevalia
Kofia ya drafti hapo katikati ni Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa
Kituo cha Redio cha Bomba FM kilichopo Jijini Mbeya Bwana Iman John
Mwakapoja akiwa eneo la tukio akiongea na wananchi walioshuhudia tukio
hilo eneo la Mama John Jijini Mbeya.
Wananchi
wakiwa eneo la tukio wakishuhudia zoezi la uokoaji wa majeruhi zaidi ya
watatu wa ajari hiyo ambao wamejeruhiwa vibaya lakini sikufanikiwa
kupata picha ambayo inaonesha vizuri kutokana na giza.
Tabia ya
kutoa namba kwa Wamiliki wa Magari mkoani Mbeya yaendelea kwa sababu
ambazo hazieleweki je?, ni kuficha ushahidi. Mpaka dakika ya mwisho
tulifanikiwa kupata jina na Anwani ya mmilikiwa gari hilo ambayo ilikuwa
imeandikwa ubavuni mwa gari hilo ambaye ni:-
Bwana Issa
John.
S.L.P 3500
Mbeya.
Tanzania.
Tanzania.
Mwananchi
mmoja anusurika kufa baada ya kubata kipigo kutoka kwa Wananchi kwa
kosa la kutaka kuiba taa za gari, Jeshi la Polisi la wahi kumwokoa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)