Waziri wa Elimu atembelea maonyesho ya nanenane mjini Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri wa Elimu atembelea maonyesho ya nanenane mjini Dodoma

Waziri wa Elimu Dkt. Jumanne Shukuru Kawambwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma mara baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma
Waziri wa Elimu Dkt. Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akiangalia jana maandishi maalum ya watu wenye ulemavu wa kutoona kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi Msaidizi wa kitengo cha Elimu Maalum Wizara ya Elimu Amani Katembo(kulia) wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma
Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akifuatilia maelezo jana kutoka kwa Afisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu Jane Kamwera(kulia) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne kulalamikia udanganyifu wanaofanyiwa na Wamiliki wa Vyuo Vya ualimu binafsi kuwa wanaweza kujiunga na Diploma ya Ualimu kwa sifa za Kidato cha Nne tu. Waziri huyo alipata maelezo hayo kwenye banda la Wizara hiyo wakati alipotembelea maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma
Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akipata maelezo jana kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi Msaidizi , Kitengo cha Elimu Maalum , Wizara ya Elimu Amani Katembo (kulia) juu ya matumizi ya mashine yakuchapa ya watu wenye ulemavu wa macho (typewriter ) wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma.
Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages