Mkuu
wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza (kulia) akiwa na
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga waandaji wa
Vodacom Miss Tanzania wakizungumza na warembo wanaowania taji la Miss
Tanzania 2011, baada ya kuwasili katika kambi yao iliyopo Hotel ya
Giraffe Ocean View Mbezi Beach jijini Dar es Salaam jana.
Waremmbo
wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya
pamoja baada ya kuwasili katika kambi yao iliyopo Hotel ya Giraffe
Ocean View Mbezi Beach jijini Dar es Salaam jana.
Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala (katikati
mwenye miwani) akigonganisha glasi ishara ya kuwakaribisha warembo
wanaowania taji la Miss Tanzania 2011 baada ya kuwasili katika kambi yao
iliyopo Hotel ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
jana.
Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya warembo 30
kutoka kanda tofauti nchini leo (jana) wameanza rasmi kambi ya Vodacom
Miss Tanzania 2011 yaliyopangwa kufanyika Septemba 10 kwenye ukumbi wa
Mlimani City kwa mfumo tofauti na ule uliozoeleka miaka
ya nyuma ambapo warembo walikuwa wakikaa kambini katika Hotel ya Giraffe
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Vodacom
Tanzania ambao ndio wadhamamini wakuu wa shindano la Vodacom Miss
Tanzania kwa miaka kadhaa mfululizo safari hii wamebadilisha kabisa
muundo wa awali na hivyo walimbwende hao watakaa ndani ya jumba maalum
lililopewa jina ‘Vodacom House’.
Mkuu
wa Udhamini wa kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema jijini Dar es
Salaam kuwa lengo la kufikiwa kwa mabadiliko hayo ni kulifanya shindano
hilo liwe na muonekano tofauti kama ilivyo kwa Vodacom ambayo imebadili
muonekano wake na kasi ya utoaji huduma.
“Safari
hii warembo 30 wanaoshiriki shindano hili la Vodacom Miss Tanzania
wataishi kwenye jumba maalum ‘Vodacom House’ na humo watafundishwa vitu
mbalimbali ikiwemo jinsi ya kukabiliana na vishawishi hususan katika
masuala ya kimapenzi,” alisema Rwehumbiza.
Akitaja
malengo mengine ya kuwaweka washiriki hao ndani ya jumba hilo Mkuu huyo
wa udhamini alisema kampuni yake kwa sasa inatoa huduma kwa teknolojia
yenye kasi zaidi hivyo warembo hawana budi kuendana nayo kwa kufundishwa
aina ya kula, kuondoa ulimbukeni mara wanapopata umaarufu.
Mabadiliko
haya yatalifanya shindano hili kuwa bora na linaloenda na wakati kama
zilivyo huduma zetu yaliyotokana na mabadiliko ya nembo yetu. Wakiwa
ndani ya jumba warembo watakaa kwa wiki tatu wakijifunza masuala ya
kijamii, alisema Rwehumbiza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Lino Agency waandaaji wa shindano hilo Hashim
Lundenga amesema kwa mwaka huu wanataka warembo wenye sifa ikiwemo
elimu, muonekano na tabia nzuri ili mshindi atakayepatikana aweze
kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa.
“Sisi
hatuangalii mshiriki ametoka wapi iwe kijijini au mjini,
tunachozingatia ni mrembo kukidhi viwango vya shindano ikiwemo sifa
tunazozitaka ili mwisho wa siku kila mtu ajivunie mafanikio aliyoyapata
akiwa ndani ya jumba la Vodacom House na atumie kigezo hicho kufanikiwa
kimaisha,” alisema Lundenga.
Lundenga
alisema kuwa mfumo wa mashindano ya mwaka huu, umebadilika ambapo jumla
ya warembo 15 wataingia hatua ya nusu fainali baadala ya 10 kama
ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alisema
kuwa kati ya warembo hao 10, watano watapatikana katika mashindano
maalum wakiwa katika Vodacom House. Kwa mujibu wa Lundenga, kutakuwa na
mashindano ya Top Model ambayo yatafanyika leo na baadaye kufuatiwa na
mashindano ya Vipaji (Talent), Mrembo bora wa muonekano katika picha
(Miss Photogenic), Mrembo bora wa michezo (Top Sports Woman) na mrembo atakayeonyesha ushirikiano mkubwa na uchangamfu katika kambi, Miss Personality.
Ili
kuishirikisha jamii, maisha ya washiriki hao wa Vodacom Miss Tanzania
2011 ndani ya Vodacom House yatakuwa yakioneshwa moja kwa moja ‘Live’ na
vituo vya Startv pamoja na Clouds TV ili kutoa nafasi kwa watazamaji
kumpigia kura mrembo anayefaa kuvikwa taji hilo na kumrithi Genevieve
Mpangala mshindi anayemaliza muda wake.
Picha Na John Bukuku - Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)