Ofisa Mkuu wa
Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, akielezea
namna ya kushiriki katika promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja
wa Kampuni ya Vodacom, kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha, wakati
wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford.
Ofisa Mkuu wa Masoko
na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari kuhusu promosheni hiyo Mpya ya Mega
inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha.
*******************************************
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imetangaza promosheni mpya ya aina yake kwa wateja wake nchi nzima ambao
wataweza kujishindia zawadi ya shilingi milioni kumi na moja pamoja na
televisheni za kisasa aina ya Samsung LCD mia moja kila siku kwa siku
mia moja.
Akitangaza promosheni hiyo
iitwayo Mega Promotion jijini Dar es salaam Afisa Mkuu wa Masoko na
Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba amesema promoheni hiyo ni
kubwa kuwahi kuendeshwa na Vodacom tangu ilipofanya mabadiliko makubwa
ya kimuono na falsafa mapema mwaka huu yaliyohusisha mabadiliko ya rangi
kutoka buluu kuwa nyekundu pamoja na nembo ya kampuni.
Mwamvita amesema promosheni
hiyo itadumu kwa siku mia moja kuanzia Agosti 26 hadi Desemab 6 mwaka
huu na ili kushinda mteja wa Vodacom atapaswa kujiunga katika shindano
la kujibu maswali kupitia simu yake ya mkononi ambapo kupitia majibu ya
maswali hayo mteja atakuwa akijikusanyia pointi zitakazoshindanishwa
kwenye droo za kila siku.
"Vodacom ni ya kwanza kuleta
promosheni ya aina hii, nasema hivi kwa sababu Mega Promosheni inampa
mteja fursa ya kuchagua hatua ya ushiriki. Ushiriki wa BURE wa droo za
Standard ambapo mteja hujiunga BURE na kuwa na nafasi ya BURE kushinda
televisheni moja ya kisasa aina ya Samsung LCD kila siku na hatua
nyengine ni ya droo za Premium ambapo mteja atajiunga kwa gharama NAFUU
ya shilingi mia tano na hamsini kwa siku kuwania kitita cha shilingi
milioni kumi na moja kila siku" Alisema Mwamvita.
Mwamvita ameongeza kuwa ili
kushiriki droo ya bure mteja atapaswa kutuma ujumbe mfupi wa neno BURE
ama FREE kwenda nambari 15015 na mara moja atapokea swali la kwanza
litakaloanza kumpatia pointi ambazo mwisho wa siku zitashindanishwa
katika droo ya wazi itakayooneshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya
ITV kila siku saa moja na dakika hamsini na tano usiku.
Burudani ya aina yake katika
promosheni ya Mega ipo katika droo ya Premium ambayo kupitia droo za
kila siku inatoa mshindi mmoja wa zawadi ya kitita cha fedha taslimu
shilingi milioni kumi na moja.Hata hivyo mteja ana uhuru wa kuchagua
kuondoa ushiriki wake katika droo hii wakati wowote.
"Ifahamike kuwa mshiriki wa droo hii ya Premium
kwanza lazima ujiunge na hatua ya kwanza ambayo ni ya BURE kuwania
televisheni kupitia droo ya Standard na baada ya hapo mteja atakuwa na
uamuzi wa kuendelea na hatua ya Premium ambapo mbali na kushiriki na
kushinda zawadi ya fedha bado anakuwa na mshiriki wa droo ya Standrd
hivyo anaweza kushinda zawadi mbili kwa mpigo"Alifafanua Mwamvita.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Promoheni hiyo ya Mega Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja wa Vodacom Charity Safford amesema Vodacom ina imani kwamba promosheni hiyo itawavutia wateja wake hasa kutokana upekee ilionao.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Promoheni hiyo ya Mega Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja wa Vodacom Charity Safford amesema Vodacom ina imani kwamba promosheni hiyo itawavutia wateja wake hasa kutokana upekee ilionao.
"Wateja wetu ni kipaumbele
chetu cha kwanza kabisa na daima tunajituma kuhakikisha tunawapa huduma
bora zaidi kuweza kukidhi mahitaji yatokanayo na shughuli zao za kila
siku na kwa mara nyengine tunawaomba watanzania wafurahie hiki
tunachowatangazia sasa ambapo kunatoa fursa ya kushinda zawadi kwa kila
mmoja aliye tayari kujiunga kwa kulipia au hata yule ambae hayupo tayari
kujiunga kwa kulipia lakini anapenda kushinda zawadi"





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)