Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala, akizungumza na
wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali,
Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki katika harakati za kutatua
mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo, kufuatia mwekezaji Raia
wa kigeni kuuziwa
eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao na kufunga barabara,
shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho. Picha na Mroki Mroki
Mbunge wa
Jimbo la Mvomero, Mkoani Morogoro, Amos Makala (kushoto) akikagua
uzio uliowekwa na Kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa na
Mzungu aliyenunua shamba Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera,
Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero na kuzua mgogoro mkubwa wa mipaka
baina yake na wananchi wa eneo hilo. Anayemuongoza ni Said Ahmad mkazi wa Kinyenze.
Wananchi wa Kitongoji
cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero,
wakiwa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la
Mvomero, Amos Makala aliyefika kijijini hapo mwishoni mwa wiki
kufuatilia mgogoro wa ardhi ulipo kati ya wananchi hao na mwekezaji raia
wa kigeni aliyenunua shamba kijijini hapo na kuweka uzio na kufunga
njia na mashamba yao.
***********************************************************
***********************************************************
*Atoa wiki
moja maofisa ardhi kumaliza tatizo au kutinga Mahakamani
Na Mroki Mroki, Mvomero
MBUNGE wa jimbo la Mvomero,
mkoani Morogoro, Amos Makala, ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo
baina ya Mwekezaji na Wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze , Kijiji cha
Kipera, Tarafa ya Mlali , Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Akizungumza mwishoni mwa wiki
Kijijini hapo, Makala aliyeambatana na Ofisa Ardhi wa Wilaya hiyo,
Majaliwa Jaffari ameiagiza idara ya ardhi kuchukua hatua za haraka na
dharula kutatua mgogoro huo kabla ya kuibuka kwa machafuko ya uvunjifu
wa amani.
Kwa Habari Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)