WASHIRIKI WA VODACOM MISS TANZANIA 2011 KUPAMBANA LEO KATIKA BONANZA LA MICHEZO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASHIRIKI WA VODACOM MISS TANZANIA 2011 KUPAMBANA LEO KATIKA BONANZA LA MICHEZO

Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom

NA LYSBERT MORAGWA, SAUT

WAREMBO wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, kesho wanatarajia kuchuana katika kuonyesha vipaji vyao katika michezo, kwenye ufukwe wa Jangwani Sea Breeze, Dar es Salaam.
Tukio hilo litakaloanza saa 3:00, ni miongoni mwa vipengele (fast tracks) vitano vya awali vya kinyang’anyiro hicho ambapo washindi hutinga moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali.

Tayari warembo wawili wameshapata tiketi ya kuingia nusu fainali ya mashindano hayo ambao ni Mwajabu Juma aliyeshinda taji la Top Model na Tracy Sospeter aliyeshinda taji la Miss Photogenic.
Mbali ya vipengele hivyo, vingine vilivyobaki ni Kipaji (Talent) na Mvuto (Personality) ambapo mshindi wake hutangazwa kila wiki kabla ya fainali za taifa zilizopangwa kufanayika Septemba 10, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga, michezo itakayohusishwa leo ni riadha, mbio za magunia, kuogelea, kuruka chini, mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba na mingineyo. 

Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, limedhaminiwa na Vodacom, Redd’s Original, New Habari (2006) Ltd, Star TV, Giraffe Hotel na Papa Zee Entertainment.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages