Raisi Jakaya Kikwete
Na Nova Kambota,
Ndiyo Ikulu yako mpendwa rais wangu Jakaya Kikwete imetumbukia kwenye “sifa kashfa” ya kumsafisha David Jairo eti magazeti yamepambwa na kichwa hiki “Ikulu Yamsafisha Jairo” . Pengine wewe mheshimiwa Kikwete unajisikiaje labda baada ya Ikulu yako kumsafisha Jairo? au Luhanjo anasema nini sasa?
“Silence means Yes” au? kama siyo kwanini basi Ikulu yako ipo kimya? Mpendwa rais wangu umeshiriki kumsafisha Jairo! mmmh! HONGERA SANA NASEMA TENA HONGERA SANA!
Msafi haitaji kusafishwa bali mchafu anahitaji……………………………kama Ikulu yako ilivyofanya! SAFI SANA RAIS WANGU! Tanzania itakukumbuka kwa mengi lakini la Ikulu Yako kumsafisha Jairo HAKIKA BIG UP RAIS WANGU.
Haya twende tu kwani mbona nimekuzoea hata jamaa zangu pale kijiweni eti wanakutania kuwa “umeshindwa kujivua gamba eti limeishia kiunoni” teh teh teh! mmh kazi sasa ipo kwa makamu wako kwenye chama “The Annointed Comrade Pius Msekwa ” duuh kwa yaliyovumbuliwa huko Ngorongoro kumbe na yeye ni gamba aisee! POLE SANA RAIS WANGU UMEZUNGUKWA NA MAGAMBA, what about you my prezda?
Nasema haya ooh tusije kulaumiana tu nakwambia rais wangu NARUDIA TENA usije kusema sijakupa pongezi kwa KUMSAFISHA JAIRO, ooh! nasema HONGERA SANA MJOMBA , lakini najaribu kuwaza juu ya uwezo wako wa kupambanua mambo rais wangu Kikwete, NAULIZA HIVIIII….Je unafahamu tofauti ya ngwara na mtama? je wewe kwa kumsafisha Jairo umejipiga nini? mtama au ngwara?…. SORRY RAIS WANGU NAWAZA TU KWA SAUTI LEO! Nova Kambota Mwanaharakati,Nipigie +255717 709618Niandikie novakambota@gmail.comNitembelee www.novakambota.com 27 August 2011, Saturday.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)