Profesa Msambichaka |
Na
Lukwangule
Bodi
ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewafukuza wahadhiri 21 wa
chuo hicho kutokana na kuendesha mgomo unadaiwa sio halali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana Profesa Lucian
Msambichaka, amesema uamuzi huo ulifikiwa Agosti 17, mwaka huu baada ya
kufanyika kwa kikao cha Bodi.
Kwa mujibu wa taarifa wahadhiri hao wamefukuzwa kwa
kukaidi maagizo ya mamlaka za juu.
Agizo
la kutaka Taasisi hiyo ifunguliwe mara moja lilitolewa hivi karibuni na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye aliigiza Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii inayoisimamia Taasisi hiyo kushughulikia suala hilo mapema
iwezekavyo.
Wahadhiri
waliofukuzwa kazi ni Faustine Nzigu, Rindstone Ezekiel, Mariana Makuu,
Aziel Elinipenda, Deodatus Mkumbe, Daud Chanila, Viscal Kihongo,
Elizabeth Bitegela, Joseph Sunguya, na Constantine Njalambaya.
Wengine
ni Mwajuma Hussein, Rita Minga, Caroline Mutagwaba, Elia Kasalile,
Marwa Phanuel, Adrophina Salvatory, Kinswemi Malingo, Suzana Nyanda,
Machumbana Michereli, Warioba Nyamoni na Yassin Mwita.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)