Shughuli zikiendelea katika mgodi wa Chunya.
Wachimbaji wadogowadogo wa madini
mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwawezesha vifaa vya uchimbaji wa
madini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Ombi hilo limetolewa na mmoja wa
wachimbaji hao Bwana Daniel Mwaisabila wakati wa mahojiano kuhusu namna
ambavyo Serikali ingeliweza kuwasaidia katika shughuli zao za madini.
Amevitaja vifaa wanavyotumia kwa
ajili ya shughuli hizo za uchimbaji wa madini kuwa ni Sululu na koreo
ambavyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha ufanisi wao
wa kazi
Hata hivyo amewataka vijana kujituma katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili waweze kujikwamua dhidi ya umasikini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)