Mkurugenzi
wa Lino International Agency, waandaji wa Shindano la Vodacom Miss
Tanzania, Hasim Lundenga akitangaza matokeo ya shindi wa shindano la
Vodacom Miss Photogenic 2011. Kulia ni Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya
Kaskazini, Nguvu Kamando
Mshindi
wa taji la Miss Photogenic 2011, Tracy Sospeter akiwa katika poazi
baada ya kutajwa kuwa ndie mshindi katika shindano hilo dogo katika
shindano la Vodacom Miss Tanznia 2011 na kufanikiwa kuwa mrembo wa pili
kuingia katika hatua ya 15 bora ya shindano hilo. Mshindi huyo
alitangazwa akiwa mjini Arusha jana
Warembo
Vodacom Miss Tanzania 2011, waliofanikiwa kuingia tano boira ya
shindano la Miss Photogenic 2011 kutoka kulia , Trecy Mabula,Jeniffer
Kakolaki, Chiaru Masonobo, Christine William na Glory Lori wakipozi kwa
picha ya pamoja baada ya kutajwa kufanikiwa kuingia katika hatua hiyo
jana mjini Arusha.
=============================
Mrembo Tracy Mabula aula, ashinda taji la Vodacom Miss Photogenic.
MWANDISHI WETU, Arusha
MSHIRIKI wa Vodacom Miss Tanzania Tracy Mabula(20) ameibuka
mshindi wa taji la Vodacom Miss Photogenic baada ya kuwabwaga washiriki
wengine 29 katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika mkoani Arusha
ambapo warembo hao wapo kwa ziara ya mafunzo.
Kwa
ushindi huo, mlimbwende tracy anayewakilisha mkoa wa Shinyanga, sasa
atatumiwa na Vodacom Tanzania katika matangazo mbalimbali na tayari
ameingia katika nafasi robo fainali .
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando amesema ushindi wa
mrembo huo ni ishara kwamba ana muonekano unaoendana na utendaji wa
kampuni hiyo unaofanya kazi kuendana na wakati uliopo.
“Mara
nyingi tumekuwa tukitumia mawakala kututafutia watu wa kufanya
matangazo ya bidhaa na kazi zetu mbalimbali, ni matumaini kipindi hiki
Tracy atatuwakilisha vema katika kazi zetu na kuifikisha Vodacom
inapotaka,” alisema Kamando.
Naye
Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ndio waandaaji wa Vodacom Miss
Tanzania Hashim Lundenga alisema kitendo cha mshiriki huyo kuvikwa taji
hilo ni kiashiria tosha kwamba shindano la Vodacom Miss Tanzania sio
uhuni kama baadhi ya watu wanavyoliita.
“Baadhi
ya watu wamekuwa wakiliita shindano letu kwamba linalokiuka maadili ya
Kitanzania, kwa kitendo cha kampuni ya Vodacom kutuamini na kumchagua
mmoja wa washiriki wetu kuwa balozi wao kinadhihirisha kazi yetu
imelenga kuisaidia jamii katika kujiletea maendeleo,” alisema Lundenga.
Mbali
na hayo Lundenga alimuomba mrembo huyo kuiwakilisha vema kamati ya Miss
Tanzania huko aendako ili kutoa fursa kwa warembo wengine kuweza
kutumiwa na kampuni hiyo jambo litakalowakomboa wanawake wa Kitanzania.
Kabla
ya tracy kutangazwa mshindi, warembo wengine wane ambao waliingia
fainali katika shindano hilo, ambao walitangazwa na Lundenga ni pamoja
na Jeniffer Kakolaki,Christina William, Glory Lory na Zerulia Manoko.
“nimefurahi
sana baada ya kushinda nafasi hii, na nina imani nitaitumia vizuri
katika kutangaza kazi za Vodacom na nyingine ambazo ntapangiwa na kamati
ya Miss Tanzania”alisema Tracy.
Kabla
ya shindano hilo washiriki wa shindano hilo mwaka huu waliendelea na
ziara hiyo kwenye Mikoa ya kanda ya Kaskazini na kupata fursa ya
kutembelea kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe
Sokoine.
Wakiwa
eneo la Monduli warembo hao walipokelewa na Mtoto wa Sokoine Nameloki
Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Arusha
aliyekuwa mgeni rasmi.
Akizungumzia
ziara hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwa Njia ya Mtandao wa Vodacom
Tanzania Matina Nkurlu alisema washiriki hao wanajifunza vitu mbalimbali
ikiwemo utalii wa ndani na rasilimali zilizopo nchini.
Mwaka
huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo tofauti na uliozoeleka
kwani wamewekwa kwenye jumba maalum la ‘Vodacom House’ ambapo matukio
yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Startv na Clouds TV na watazamaji
watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)