Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania, Angetile Osiah. |
Mechi
ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon
katika ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert
Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza.
Awali
tulipanga mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini
uamuzi wa kuihamishia Mwanza umefanyika baada ya jana kupata barua
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikitufahamisha
kuwa Uwanja wa Taifa hautatumika tena kwa sasa. Kwa mujibu wa Wizara,
uwanja huo utakuwa katika matengenezo baada ya kuharibika wakati wa
michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita.
YANGA, SIMBA NAZO KUATHIRIKA
Uamuzi
huo wa uwanja kufungwa kwa ajili ya matengenezo pia umeziathiri klabu
za Yanga na Simba ambazo zilikuwa zimekubaliwa timu zao zitumie kwa
ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inaanza kutimua vumbi
Agosti 20 mwaka huu.
Tayari
leo (Agosti 18 mwaka huu) tumeziandikia rasmi klabu za Simba na Yanga
kuzifahamisha kuhusu uamuzi huo wa Wizara, hivyo kuzitaka zitafute
viwanja vingine kwa ajili ya mechi zao za ligi.
Hatua
hiyo ya uwanja kufungwa, itailazimisha TFF ifanye mabadiliko kwenye
ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuzingatia viwanja ambavyo klabu za
Yanga na Simba zitakuwa zimeamua kuvitumia.
Mabadiliko
hayo pia yataziathiri timu za African Lyon, Azam, JKT Ruvu, Moro United
na Villa Squad ambazo licha ya kutumia Uwanja wa Azam ulioko Chamazi,
Dar es Salaam, zilipanga mechi zao za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga
zichezwe Uwanja wa Taifa.
Kwa
sasa msimamo wa wamiliki wa Uwanja wa Azam ni Yanga na Simba kutoutumia
kwa vile uwezo wake wa kuchukua watazamaji ni mdogo.
Boniface Wambura,
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)