Takriban watu 14 wamekufa katika
eneo la Kaskazini Mashariki katika eneo la Turkana nchini Kenya, vifo
vya kwanza kutokea vinavyohusiana na njaa nchini Kenya katika eneo
linalohusiana na ukame.
Mbunge wa Turkana, John Munyes, alisema vifo
hivyo vimetokea katika vijiji vitatu baada ya serikali kushindwa
kusafirisha chakula kwa ajili ya watu walioathiriwa na ukame.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya raia wa Kenya
milioni nne wanatishiwa na ukosefu wa chakula katika eneo lilikumbwa na
ukame mbaya katika kipindi cha miaka 60.
Nchi nyingine zilizoathiriwa ni Somalia, Ethiopia na Djiblouti.
Mwandishi wa BBC Odiambo Joseph akiwa Turkana
anasema ametembelea kijiji ambacho mamia ya watu wengi wao wakiwa wazee
na dhaifu walikuwa kwenye mstri mrefu wa kugawiwa chakula.
Watu 14 waliokufa nchini Kenya walikuwa watu wazima, lakini watoto pia wana utapiamlo mkali, mwandishi wa BBC anasema.
'Watu wanahisi wametelekezwa'
Bw Munyes, ambaye ni Waziri wa Kazi katika
serikali ya Muungano ya Kenya, alisema idadi ya vifo ingekuwa juu kama
Shirika la Msalaba Mwekundu lisingekuwa linagawa chakula cha msaada
Turkana.
"Ingekuwa ni janga," alisema. Bw Munyes alisema vifo hivyo havikusababishwa na upungufu wa chakula bali ni ‘ukosefu wa utaratibu.’
Serikali imeshindwa kusafirisha chakula kwenye vijiji hivyo, alisema.
Mwandishi wa BBC anasema watu wengi Turkana
wanahisi wametelekezwa na wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuiangalia
kwa makini hali yao mbaya. Umoja wa Mataifa unasema ukame umesababishwa na ukosefu wa mvua kwa miaka mingi mfululizo.
Umetangaza rasmi kuwa sehemu kadhaa za Somalia zinakabiliwa na njaa.
Karibu raia 1,300 wa Somalia wengi wao wakiwa
wanawake na watoto wanaingia nchini Kenya kila siku wakitafuta chakula,
Umoja wa Mataifa unasema.
Source: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)