Waalikwa wakiomba dua baada ya kufuturu katika ubalozi wetu London, Ijumaa
Naibu Balozi Mh. Chabaka Kilumanga akitoa shukrani na neno kwa waalikwa
Sehemu ya wageni
Afisa ubalozi Bw. Zamarani akikaribisha wageni kufuturu |
Baadhi ya waalikwa kinama wakifuturu |
Mkuu wa utawala na fedha ubalozini hapo Da'Carol Chipeta (shoto) akipozi
na Da' Jestina George
Asalaam Aleikhum,
Ubalozi
wa Tanzania Hapa London Ijumaa uliwaalika watanzania kutoka madhehebu
na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni
ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu. Vyakula vya aina
mbalimbali viliandaliwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh
Chabaka Kilumanga aliwashukuru wadau wote ambao walioweza kujumuika na
kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Kilumanga aliahidi kushirikiana na
watanzania kwa ukaribu zaidi kwa hali na mali pia kuwaomba kutoa
ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa
kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema
Ubalozi upo kwa ajili ya wote hivyo kila mtu na autumie ipasavyo.
Kwa
niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati
kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na
kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.
Asanteni Sana,
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
URBAN PULSE CREATIVE
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)