Warembo
wanaoshiriki katika shindano la kumsaka TOP Model wa Vodacom Miss Tanzania,
wakipita mbele ya majaji wakati wa shindano hilo, ambapo warembo watano
walifanikiwa kutinga hatua ya 5 bora katika shindano hilo lililofanyika usiku wa
kuamkia leo katika Hotel ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam. Mshindi wa
taji la TOP MODEL atajinyakulia tiketi ya moja kwa moja ya kuingia Nusu Fainali
ya Vodacom Miss Tanzania 2011.
Washiriki wakipia mbele ya majaji wakati wa shindano
hilo.
Warembo hao washiriki wakipozi kwa picha wakati
wakisubiri matokeo.
Mshiriki akionyesha manjonjo yake na umahiri wa 'Cat
Walk' wakati wa shindano hilo.
Majaji wa shindano hilo wakiwa bize kupata pointi za
washiriki.
Warembo 5 kati ya 30, wanaowania taji la Vodacom Miss
Tanzania 2011, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya kumsaka mkali
atakayetwa taji la TOP Model, wakipozi katika picha baada ya
kutangazwa.
Mshiriki akipita mbele ya majaji wakati wa shindano
hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)