KWA kawaida kwenye maisha hata uendeshaji wa nchi kuna siri kubwa
lakini kwa hili la sasa hakuna tena usiri bali ni ukweli kuwa rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia
ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,CCM amejiapiza kuongeza ulinzi kwa
kiongozi mkuu wa upinzani nchini na katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Wilbroad
Slaa.
Ingawaje taarifa ambayo kwa mara ya kwanza inachapwa kwenye tovuti hii lakini ukweli utabaki hivyo kuwa kutokana na umaarufu unaozidi kukua wa Dr Slaa, huku pia idadi yake ya maadui ikikua kwa kasi pia wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamemtaka rais Kikwete kuhakikisha kuwa mwanasiasa huyo hadhuriwi na mtu kwa madai kuwa jambo lolote baya dhidi yake linaweza kuleta hali ya vurugu nchini au taharuki kutoka kwa maelfu ya wafuasi wake.
Hali hii imemshawishi rais Kikwete na serikali yake kuongeza ulinzi kwa kiongozi huyo huku taarifa zaidi zikibainisha kuwa licha ya kuwa mwanasiasa lakini pia Dr Slaa ni raia kama watanzania wengine na anahitaji ulinzi wa maisha yake pia.
Tovuti hii inatoa wito kwa watanzania wenye tabia ya kubisha pasipo hoja au utafiti kufanya upelelezi kwenye mikutano ya Dr Slaa na misafara yake ndipo watabaini ni jinsi gani uongozi wa rais Kikwete unafanya kazi ya kumlinda kikamilifu Dr Slaa ili asidhuriwe na wabaya wake.
Habari Na Nova Kambota
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)