![]() |
Boniface
Wambura
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
|
Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi
ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika
mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na
Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani ni sh.
3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000,
VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza
kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.
Taifa Stars tayari iko
kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi
Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana
na kuanza mazoezi jioni.
Wachezaji wan je
waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na
Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa
(Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo
jioni.
Nizar Khalfan wa
Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho
kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege
ya PrescisionAir akitokea Nairobi.
TWIGA STARS KUAGWA KESHO
Timu ya Taifa ya
wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka
huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games
itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa
kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Twiga Stars wataagwa
saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai,
Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface
Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.
Wachezaji hao ni Sophia
Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma
Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester
Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi,
Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.
Viongozi watakaofuatana
na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu
Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.
Mechi ya kwanza ya
Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili
dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars
itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka
huu dhidi ya Zimbabwe.
KIM AITA 30 TIMU YA VIJANA
Kocha wa timu za vijana
Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya
mazoezi mwezi ujao.
Wachezaji walioitwa ni
Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar),
Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew
Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba),
Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT
Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC
Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).
Wengine ni Simon Msuvan
(Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim
Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC),
Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba),
Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza),
Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu
Shooting).






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)