![]() |
| Joha Kassim, akiimba wakati wa mazoezi na kundi lake jipya la T-Moto Morden Taarb. |
![]() |
| Mrisho Rajab, mshiriki wa BSS 2011, akighani rap zake zitakazotumika katika baadhi ya nyimbo hizo mpya. |
![]() |
| Hassan Ali, aliyetoka kundi la Fife Star, akiwa katika mazoezi hayo. |
*Mtoto
wa Salmini afanya kufuru, abomoa makundi ya jahazi na five star
*Asema
kundi hilo ni kama ‘Real Madrid’
*Kutambulishwa na Aliyeniumba
Hajanikosea
MTOTO wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amin
Salmin ‘Mourinho’, amenzisha kundi jipya la muziki wa Taarab
linalojulikana kwa jina la T Moto Morden Taarab ‘Real Madrid’
linaloundwa na wasanii mahiri waliopata kutamba katika makundi ya Jahazi
Morden Taarab, Five Star na mengineyo.
Akizungumza na Sufianimafoto, Amin
alisema kuwa ameamua kuleta mabadiliko na ushindani katika muziki wa
taarab kutokana na muziki huo kutokuwa na makundi yenye ushindani wa
kisanii zaidi ya majungu na kufanya baadhi ya makundi yakivunjika kwa
kushindwa kutoa upinzani na kubuni vitu vipya vinavyoweza
kusaidia kulibakiza kundi katika jukwaa la muziki huo.
Aidha alisema kuwa ni siku nyingi
alikuwa na ndoto ya kumiliki kundi la muziki wa Taarab, kutokana na
kuvutiwa zaidi na muziki huo, lakini amekuwa akisikitishwa na baadhi ya
wanamuziki wa taarab wanaopotea na vipaji vyao ama kushindwa kuwa na
maisha mazuri hali ya kuwa wanakuwa wamefanya kazi kubwa ambayo hutokea
kupendwa na mashabiki na kuuzika.
Amini anayejiita Mourihno kutokana na
‘kusajili’ wanamuziki nyota kutoka katika makundi makubwa ya muziki huo
amesema kuwa wanamuziki aliowapata kuunda kundi hilo, anatarajia kuwa
kundi hilo litafanya mambo mazuri na makubwa yatakayowashitua mashabiki
wa muziki huo kwa kipindi kifupi kutokana na umahiri wa
wanamuziki hao wenye hari zaidi na morari ya kufanya kazi kwa mageuzi na
maslahi.
“Kutokana na kuuelea vyema muziki huu,
kundi letu tumeamua kutumia aina ya kipee kati ya makundi yote
yanayopiga muziki huu kwa kutumia jumla ya magitaa matatu ili kuweza
kuleta radha na vionjo tofauti vya muziki huu, tofauti na makundi
mengine ya taarab ambayo hutumia magitaa mawili tu” alisema Amini.
Aliwataja wanamuziki wanaounda kundi
hilo jipya kwa upande wa waimbaji kuwa wanaongozwa na mwanamuziki
mkongwe, Mwanahawa Ali, Mosi Suleiman aliyetoka kundi la
Dar Morden Taarab, Joha Kassim, kutoka kundi la Five Star, Hasina
Kassim, kutoka kundi la New Zanzibar Morden Taarab, Hassan Ali kutoka
kundi la Five Star na Mrisho Rajab mshiriki wa BSS 2011.
Kwa upande wa wapiga vyombo wanaongozwa
na mpiga Solo, Jumanne Ulaya ‘Mkono wa Biashara’ aliyetoka kundi la
Jahazi Morden Taarab, Wapiga kinanda ni pamoja na Amour Saleh
Zungu, aliyewahi kupita katika bendi za Twanga Pepeta, TOT na
nyinginezo, Moshi Mtambo, kutoka kundi la New Zanzibar
Morden Taarb na Omary Kisila kutoka, wengine
ni pamoja na mpiga gitaa la rythim, Fadhili Ali Mnara, aliyekuwa katika
muziki wa dansi katika baadhi ya Hoteli na mpiga Gitaa la Besi, Rajab
Kondo kutoka kundi la New Zanzibar na Mussa Mipango, nayefanya kazi kwa
mkataba kutoka kundi la TOT.
Aidha Amini alisema kuwa Kundi hilo hivi
sasa bado linaendelea kujifua kuandaa vitu vipya ikiwa ni pamoja na
nyimbo sita ambapo nne kati ya hizo zitaitambulisha albam
yao ya kwanza itakayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea,
uliotunga na kuimbwa na Bi Mwanahawa Ali.
Nyimbo nyingine ni, Mtoto wa Bongo,
inayoimbwa na Hassan Ali, Unavyojizani Mbona Hufanani, inayoimbwa na
Joha Kassim, Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake Imefika, inayoimbwa na Mrisho
wa BSS, Mwenye Kustili Mungu na kumbe Wewe ni Shoti zote
zikiimbwa na Mosi Suleiman, ambapo moja kati ya hizo itakuwa katia albam
ya.
Kundi hilo limeingia Studio leo Agosti
29 kwa ajili ya kuanza kurekodi nyimba zake mpya ambazo kwa pamoja
zitaanza kusikika hivi karibuni.
Naye kiongozi wa kundi hilo, Jumanne
Ulaya ‘Mkono wa Biashara’, aliwataka wapenzi wa miondoko hiyo ya Taarab,
kukaa mkao wa kula wakisubiri vitu vipya kutoka kwa kundi hilo vyenye
utofauti mkubwa na ambavyo vitakuwa na radha ya kutochosha kusikiliza.
“Nawaahidi tu wapenzi wa muziki wa
Taarab wakae mkao wa kula wasubiri kusikia kilichotuingiza kambini na
nyimbo ambazo kwa kweli hazichoshi kusikiliza, kwani tumetua kundi hili
kikazi zaidi na majungu” alisema Jumanne








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)