Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akimsiliza jambo Mtoto Hamadi Hassan wa darasa la Nne Skuli
ya msingi Daya Mtambwe,mara baada ya kukitembelea kituo cha ununuzi wa
zao la Karafuu cha Daya Mtambwe,pia kuzungumza na wakulima wa zao hilo
jana,katika Wilaya ya Wete jana.(13/08/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk
Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakijumuika na
wakulima wa zao la kafuu kuchambua karafuu zilizochumwa katika kambi ya
karafuu Daya Mtambwe,akiwa katika ziara ya kutembelea kambi za
wachumaji wa karafuu,Mkoa wa Kaskazini Pemba.(13/08/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk
Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiangalia magunia
ya karafuu zilizonunuliwa katika kituo cha ZSTC Daya Mtambwe jana
walipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho pamoja kambi za wachumaji wa
Karafuu,Wilaya ya wete jana,(kushoto) Naibu Mkurugenzi wa ZSTC Pemba
Hamad Khamis Hamad,(13/08/2011)
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed
Shein,akijumuika na waislamu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
katika Futari maalum aliyowaandalia waislamu hao jana katika viwanja
vya Ikulu ya Wete.(13/08/2011)
Baadhi ya Magunia ya karafii 31 yaliyokamatwa
yakiwa katika banda la ZSTC katika bandari ya Wete chini ya Ulinzi
mkali ikiwa bado hatua za kuwatafuta wahusikka zinafanywa.(13/08/2011)
Baadhi
ya wakulima wa zao la karafuu wakisubiri kuuza karafuu zao katika
kituo cha ununuzi wa zao hilo huko Daya Mtambwe,Wilaya ya Wete Mkoa wa
Kaskazini Pemba,wananchi wengi wamehamasiki kufika katika vituo mbali
mbali kuuza karafuu.(13/08/2011).Picha na Ikulu-Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)