RAIS
mstaafu Alhaj Ali Hassani Mwinyi akimkabidhi msaada wa Chakula,
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Ngozi (Albino) katika Wilaya ya
Temeke, Bw. Kassim Kigwe katika hafla fupi iliyofanyika leo (jana)
katika shule ya Sekondari Manzese Jijini Dar-Es-Salaam
RAIS
mstaafu Ali Hassani akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu wa
Ngozi Tanzania Bi. Ziada Ali Sembo (hayupo picha) wakati alipokuwa
akitoa shukrani kwa niaba ya watu wenye ulemavu katika hafla fupi ya
kukabidhi chakula cha msaada kwa kundi hilo.
RAIS
mstaafu Ali Hassani Mwinyi akizungumza na wananchi (hawapo pichani)
katika hafla fupi ya kukabidhi chakula cha msaada kwa makundi
yasiyojiweza katika jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika leo
Dar-Es-Salaam, Rais Mwinyi alikabidhi viroba (vifurushi) 224 vya vyakula
vyenye thamani ya Tsh Milioni 15.
RAIS
mstaafu Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi
ya Rehema, Bw. Abdi Adam wakati alipokuwa akitoa risala fupi ya taasisi
hiyo. Watatu kutoka kwa Rais mstaafu ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Bi.
Alshaymaa Kweir na anayemfuatia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu wa
Ngozi Tanznia, Bi. Ziada Ali Sembo.
Picha zote na Anna Titus - Maelezo
Picha zote na Anna Titus - Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)