Mwenyekiti
wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete (kulia) akiwakabidhi zawadi
baadhi ya walimu wanafunzi saba kutoka Tawi la Chuo cha Ualimu St.
Augustine tawi la Mtwara leo mchana walipokwenda kumuaga ofisini
kwake baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya
mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA Mkoa wa Pwani,.(katikati ni Mwalimu
mwanafunzi, Kaiza Magoa na (kushoto) Kiongozi wao Victoria John.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia alievaa baibui)
akizungumza na walimu wanafunzi kutoka chuo cha Ualimu St. Augustine
tawi la Mtwara waliofika ofisini kwake leo mchana kwa ajili ya kumuaga
baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto
yatima WAMA -NAKAYAMA iliopo chini ya Taasisi ya WAMA.
Mama
Salma akiwa katika Picha ya pamoja na walimu wanafunzi kutoka chuo cha
ualimu ST. Augustine, tawi la Mtwara waliokwenda kumuaga ofisini kwake
leo baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo kwenye shule ya
mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayofadhiliwa na Taasisi ya WAMA
huko Rufiji mkoa wa Pwani.
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)