Mbunge Mussa Khamisi Silima, alifariki dunia leo saa tano asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alihamishiwa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu
zaidi.
Taarifa
za kifo cha Silima zilitangazwa jana saa 5.50 asubuhi na Spika wa
Bunge, Anne Makinda wakati wabunge wakiendelea kuchangia makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/2012.
"Waheshimiwa
wabunge, kama mtakumbuka jana niliwatangazia kwamba, mheshimiwa Mussa
Hamisi Silima, alipata ajali mbaya eneo la Nzuguni, ambapo mke wake,
Mwanaheri Twalib alifariki dunia hapo hapo.
"Aidha
niliwaarifu kuwa, mheshimiwa Silima na dereva wake walipata majeraha
makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Leo asubuhi kabla
ya maswali,nimetoa taarifa kwenu kwamba nimeongea na mheshimiwa Silima
akiwa anaendelea kupata matibabu. Ni kweli nimeongea naye.
"Kwa
masikitiko makubwa, nawatangazieni kuwa, nimepokea taarifa kutoka kwa
katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwamba, mheshimiwa
Mussa Hamisi Silima amefariki dunia muda mfupi tu uliopita.
"Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007, ninaahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi," alisema. Kufuatia msiba huo, Spika Anne aliwataka wabunge wasimame kwa dakika moja kwa heshima ya mbunge huyo.
Spika
alisema kwa kipindi cha siku tatu, familia ya Silima imekumbwa na
matatizo makubwa, kufuatia kutanguliwa na msiba wa kaka wa mkewe kabla
ya mkewe naye kufariki dunia. Katika ajali iliyotokea jana eneo la
Nzuguni, mke wa mbunge huyo, Mwanaheri alikufa papo hapo eneo la ajali
wakati dereva wake, Chizali Sembonga, aliyekuwa akiendesha gari aina ya
Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 509 AGC
alijeruhuwa.
Silima
na mkewe walipatwa na ajali hiyo walipokuwa wakirejea Dodoma.
Mbunge huyo alikuwa amekwenda Zanzibar kuhudhuria maziko ya kaka wa
mkewe, Mwanaheri. Mbunge huyo na dereva wake walisafirishwa kwa ndege
juzi kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mwili wa
Mwanaheri ulizikwa juzi alasiri. M/mungu Awajalie Makaazi Meema Peponi
Amin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)