Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali
mstaafu, Silas Peter Mayunga, aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kuagwa kwa
mwili wa marehemu Mayunga imefanyika leo , katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini
Dar es Salaam.
Mmoja kati ya askati wa Jeshi la Uganda aliyefika katika
kuwakilisha wenzake wa Uganda, akiweka saini katika kitabu hicho cha
maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha
maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali mstaafu , Silas Peter Mayunga,
aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kuagwa kwa mwili ya marehemu Mayunga
imefanyika leo , katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakibeba Jeneza
lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi, wakipita mbele
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Viongozi wa
Serikali, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye
Kambi ya Jeshi Lugalo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa
Marehemu Luteni Jenerali staafu, Silas Peter Mayunga.
Rais wa Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akitoa
heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali
mstaafu, Silas Peter Mayunga.
Kwa Picha Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)